Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika hivi katika ukurasa huo wa Instagram: 'Jana jioni nilimlaki "Anwar Gargash", Mshauri wa kidiplomasia wa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE ) ambapo pamoja na kugusia kuhusu uhusiano wa nchi mbili na masuala ya kikanda, nilipokea pia barua kutoka kwa Rais wa Marekani.'
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana asubuhi alisema katika kikao cha serikali kuhusu kutumwa barua ya Rais wa Marekani kwa Iran kwamba: Barua hiyo bado haijatufikia lakini inatazamiwa kuwa mjumbe kutoka nchi moja ya Kiarabu ataikabidhi Tehran barua hiyo ya Trump.
Awali Rais Donald Trump wa Marekani alisema katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox Business kwamba amemtumia barua kiongozi mkuu wa Iran.
342/
Your Comment